Karibu katika shule ya kimataifa Isamilo
Yenye Mahitaji Linganifu

YANAYOTUHUSU
Shule ya Kimataifa Isamilo-Mwanza ni shule kongwe inayotumia mtaala wa Uingereza iliyoanzishwa mwaka 1956, yenye mandhari ya ufukwe unaovutia wa ziwa Viktoria katika jiji la pili kwa ukubwa Tanzania.
Tunajivunia jamii yetu yenye tamaduni tofauti zenye umoja.
Waweza kutafuta zaidi kuhusu kile tunachokifanya...
TAALUMA
Tunatumia mtaala wa Uingereza ‘Cambridge’ kwa ngazi zote kuanzia shule ya awali, msingi na sekondari. Tuna rekodi kubwa na yenye mafanikio katika mitihani ya darasa la sita, kidato cha pili, cha nne na cha sita.
Unaweza kufuatilia zaidi kuhusu mtaala tunaoutumia hapa katika shule ya awali, msingi na sekondari.


MAISHA YA MWANAFUNZI
Vilabu, michezo na sanaa ni tunu kubwa inayowakilisha shule ya kimataifa Isamilo kwa kuwapa wanafunzi fursa za kushiriki na kugundua hisia zao.
Wanafunzi wetu wanashindana kimataifa katika michezo na muziki, baadhi ya wanafunzi wetu wamo katika timu ya Taifa ya kuogelea Tanzania.
JAMII
Wanafunzi wetu wana juhudi na hujihusisha katika mambo ya shule na ya jamii inayowazunguka na wanajitahidi kuelewa na kuchangia katika changamoto kubwa.
Shule yetu ya jumamosi ni mfano mkubwa wa juhudi zetu katika kuonesha tofauti siyo tu kwa wanafunzi wetu bali hata kwa vijana wengine katika jamii inayotuzunguka ambao wana nafasi finyu ya kupata elimu bora na pana tunayoitoa hapa katika shule ya kimataifa Isamilo.
